28 Lakini kama ninatoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekwisha kuwafikia. 29 Au inawezekanaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang’anya mali yake yote pasipo kwanza kumfunga yule mwenye nguvu? Akisha mfunga ndipo hakika anaweza kupora mali yake.

30 “Mtu asiyekuwa pamoja nami ananipinga; na mtu ambaye hakusanyi pamoja nami, anatawanya.

Read full chapter